MIPANGO YA JIKO LA JUA

 

 

Soma mipango kabisa kabla ya kuanza.

 

 

Unavyohitaji:      --sanduku kubwa moja ya karton, kama sentimeta 66 x 54 x 45

                        --karton ingine (kutengeneza mfuniko)

                        --karton ingine (kwa sakafu, 56 x 44)

                        --kisu (au makasi)

                        --gamu, lita moja (au changanya unga wa ngano na maji kama huna gamu)

                        --karatasi ya aluminum, kifungu kimoja (mita tano)

                        --mabaki ya mbao ambayo inatolewa wakati wa baada ya kupiga randa, magazeti ambayo imeowekwa vipande vidogo vidogo, n.k.

                        --kioo, karatasi ya nylon (polythene), n.k., sentimeta sawasawa ya sanduku (karibu 66cm x 54cm)  ukitumia makaratasi, utahitaji mawili

                        --mabati kwa upande jeusi moja, karibu sentimeta 52 x 40

                        --rula

                        --kalamu

                        --sufuria lenye kifuniko cheusi (tumia rangi emulsion, si glossy)

 

 

KUJENGA SANDUKU:

1.   Chora laini kila ukuta ndani ya sanduku sentimeta ishirini (20) kutoka chini na ata ingine sentimeta ishirini na tano (25) kutoka chini.  Chora laini kali, ili utaweza kukunja karton bila taabu.

 

Ikiwa sanduku liko na urefu wa kwenda juu kuliko sentimeta arobaini na tano (45), chora laini ya tatu sentimeta arobaini na tano kutoka chini.

 

2.  Kunja zile kuta mbili ndefu (sentimeta 66) kwa laini, kuanza kwa laini ya tatu, na kunja upande wa ndani ya sanduku.

 

Chora laini zingine kutoka laini ya pili juu, sentimeta tano kutoka kila upande wa karton, na kunja ndani, ili kuta zote ziwe sawa.

 

3.  Fungua kuta zile zilikua zimekunjwa na uweke na aluminum upande wa ndani.  Tumia gamu ya kutosha kushikanisa kuta na aluminum vizuri.

 

4.  Weka magazeti (ama mabaki) ndani za kuta.  Hii ni "insulation"--kuzuia joto kwenda nje ya jiko haraka.  Kunja kuta tena.

 

5.  Weka mabaki ifike urefu sentimeta saba (7) kwenda juu.  Funika na kipande cha karton.

 

6.  Funika kuta zote na sakafu kwa aluminum.  Tumia gamu ya kutosha.

 

7.  Weka mabati ndani ya jiko upande mweusi uwe ukiangalia juu.  Kama huna mabati, tumia karton iliyofunikwa na aluminum na kuwekwa rangi nyeusi.

 

KUJENGA KIFUNIKO:

Kifuniko kinaweza kutengenezwa kwa namna nyingi, lakini ni lazima kuhakikisha kwamba kimefunika vizuri.

 

8.  Baada ya kutengeneza kifuniko, tengeneza mwanya itakayofunguliwa na kufungwa kama dirisha ama mlango ya nyumba.  Iwe kubwa vile itawezekana na isifadhaishe kifuniko.

 

9.  Kunja hicho kipande kwa juu.

 

10.   Funika na aluminum upande wa ndani ya dirisha.  Weka gamu vizuri sana na weka hio kuzunguka kioo kwa upande mmoja.  Halafu gandamiza kioo ndani ya kifuniko.

 

11.  Weka mashimo matatu madogo upande moja wa kifuniko.  Weka shimo moja ndogo juu ya kipande cha juu ya aluminum kinachofunguka. 

 

12.  Weka kijiti kwenye shimo kusimamaisha kipande cha juu.

 

 

 

 

 

 

HALI YA HEWA:

                        ikiwa kuna. . .                                        jiko linapika. . .

                        jua kali                                                  haraka na vizuri sana

                        mvua                                                     halipika

                        mawingu                                               pole pole

                        upepo ama hewa baridi                           sawa sawa

                        vumbi, ukungu                                       vibaya kidogo

                        juu mlimani                                            vizuri sana

                        wakati wa mchana                                 vizuri kuliko wakati wote mwingine

 

 

 

MUDA GANI KUPIKA:

Inategemea vyakula gani, sufuria gani, na jua gani.  Lakini kwa kawaida, na jua kali:

 

VYAKULA RAHISI KUPIKA        VIGUMU  KIDOGO  KUPIKA       VIGUMU SANA KUPIKA

            (masaa mawili)                          (masaa  matatu)                        (masaa manne/ matano)

            mchele                                      kuku                                         maharagwe

            samaki                                      mboga nyingine                         mtama

            mboga za majani                       mihogo                                      choroko

            mayai                                       keki                                          nyama

            viazi                                          mkate                                       dengu

 

 

 

KUPIKA:

Pika kama umezoea.  Tumia maji ya kawaida kupika mchele na vyakula vikavu kama maharagwe, dengu, mahindi, na mtama.  Lakini, kupika vyakula freshi kama nyama, samaki, kuku, matunda, na mboga (kama viazi, viazi vitamu, karoti, kabichi, au mboga nyingine), usipike na maji kwa sababu maji ndani ya vyakula vyenyewe yanatosha.

 

Ni vigumu kunguza vyakula kwa sababu jiko hili linapika pole pole.  Weka vyakula ndani mapema halafu unaweza kwenda kazini.  Ukirudi, vyakula vimeiva bila matatizo.

 

Kama kuna dakika kumi na tano za jua kila saa moja, linaweza kupika.

 

 

 

HATARI!!!

Unapogusa sufuria--angalia!--kwa sababu zinakuwa moto sana.